Alianza Mei 22 ambapo alitupia mabao mawili mbele ya Kaizer Chiefs ilikuwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Mkapa.
Kwenye mchezo huu hatua ya robo fainali, ubao ulikamiliksa Simba 3-0 Kaizer Chiefs ila Simba ilienguliwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mchezo wa kwanza kupoteza kwa kufungwa mabao 4-0.
Alipachika mabao hayo dakika ya 23 na 55 pia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali dhidi ya Dodoma Jiji alipachika mabao mawili dakika ya 23 na 41.
Dakika 90, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 3-0 Dodoma Jiji na ikatinga hatua ya nusu fainali ambapo itamenyana na Azam FC katika mchezo wao ujao ikiwa itashinda itakutana na mshindi wa mchezo kati ya Biashara United v Yanga.
Pia Mei 29 alipachika bao moja Uwanja wa Majaliwa mbele ya Namungo kwenye mchezo wa ligi ilikuwa ni dakika ya 83 na alipachika mabao mawili kwenye mchezo wa ligi mbele ya Ruvu Shooting dakika ya 17 na 87.
Ndani ya mechi nne ambazo Bocco amecheza sawa na dakika 360 amepachika mabao 7.Katika ligi ni namba mbili kwa utupiaji akiwa na mabao 13 na kinara ni Prince Dube mwenye mabao 14 yupo zake Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment