KOCHA Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa anahitaji kuona mabosi wa timu hiyo wakimuongezea mkataba mpya kiungo wake Paul Pogba.
Kocha huyo ambaye amekiongoza kikosi chake kumaliza msimu wa 2020/21 kikiwa na pointi 74 nafasi ya pili ameweka wazi kwamba ni muhimu kikosi hicho kufanya maboresho makubwa kwa ajili ya msimu ujao.
Kwa sasa kiungo wake Pogba mkataba wake umesalia mwaka mmoja na unatarajiwa kumeguka Juni, mwakani na hivi karibuni suala lake lilikuwa linashughulikiwa na ilitajwa kuwa nyota huyo anahitaji kupata changamoto mpya.
Moja ya timu ambayo ilikuwa inapewa kipaumbele kupata saini yake ni pamoja na Real Madrid jambo ambalo limemfanya Solksajaer kusisitiza kiungo huyo aongezewe mkataba.
"Pogba yeye suala la mkataba wake kwa sasa lipo mbele ya bodi na wanatakiwa kumpatia mkataba pia.
"Tunataka wachezaji bora ndani ya kikosi chetu na hata klabu yenyewe inatambua hilo. Mpaka sasa sijajua mazungumzo yao yanakwendaje lakini wanatakiwa kujua kwamba tunahitaji wachezaji bora,".
0 COMMENTS:
Post a Comment