HIVI sasa kipa wa Yanga, Metacha Metacha hayupo kwenye kikosi hicho baada ya kusimamishwa kutokana na kuonyesha ishara isiyofaa kwa mashabiki wakati timu yake ikiwashinda Ruvu Shooting 3-2, kwenye Uwanja wa Mkapa.
Metacha alionyesha ishara ya kidole chenye tafsiri mbaya kwa mashabiki, baada ya kuzomewa kwa madai kuwa alicheza chini ya kiwango na kupelekea kufungwa mabao ambayo mashabiki walitafsiri kama uzembe.
Wakati Metacha akikumbwa na kadhia hiyo mengi yanasemwa ikiwemo kuhusishwa kwenda Simba na mashabiki wakidhani kuwa hiyo ndiyo sababu ya kipa huyo kuruhusu mabao ya makusudi na kwamba haipendi klabu hiyo kwa sasa.
Sasa meneja wa kipa huyo, Jemedari Said amefunguka mambo mapya akidai kuwa siyo kwamba mteja wake huyo haipendi klabu hiyo kwani ingekuwa hivyo angeshaondoka tangu zamani kwa kuwa mpaka sasa hajamaliziwa fedha yake ya usajili.
Mbali na hilo Jemedari alikwenda mbali zaidi akisema Metacha alicheza nusu ya msimu akiwa hajalipwa hata fedha kidogo na bado aliipambania timu.
“Siyo kweli kuwa Metacha amefanya makosa ya kinidhamu kwa sababu haipendi Yanga na anataka kuondoka.
“Kwani hadi sasa bado anawadai hela yake ya mwaka jana, mbali na hivyo alicheza nusu msimu akiwa hajalipwa fedha yoyote, hivyo hiki kinachotokea sasa hakihusiani kabisa na ishu za yeye kutajwa kuondoka Yanga.
KUHUSU KUFUNGIWA NA YANGA
“Yanga wamefanya jambo nzuri sana kuchukua maamuzi mapema, kwa sababu baada ya mechi mimi nilizungumza na Metacha na nikamwambia wazi kuwa sijapenda alichokifanya na siyo kitendo cha kiungwana.
“Na nikamwambia wazi kuwa akae tayari kwa lolote kutoka Yanga, kwa sababu hawatoweza kuvumilia kwa kuwa mimi naifahamu Yanga tofauti na watu wanavyofikiria na kwa bahati nzuri Yanga wakachukua hatua,” alisema Jemedari.
Chanzo: Championi
Dhulma huzaa misiba.Mlipe kibaruwa haki yake kabla ya kukauka jasho lake
ReplyDeleteKwa hiyo kutokulipwa pesa za usajili ndiyo sababu ya kufungisha au kutukana mashabiki?
DeleteHivyo viingilio ndo pesa ya usajili na kuendesha ligi.
Hata Mhariri aliyechapisha article hii, kwa mara ya 3 sasa, nadhan ana lake jambo; huwezi kumtakasa Metacha kwa njia hii
Haina maana ukikosa pesa ndio utukane, adabu ya wapi?
ReplyDeleteViongozi wetu yanga mnazidi kutufedhehesh. Sisi ndio klabu ya kwanza tz kuingiza madhabiki wengi viwanjani. Achilia mbali mauzo ya jezi. Pesa mnakula. Wachezaji wanahangaika. Oneni aibu
ReplyDeleteKatukana kutokana na zomeazomea zetu na cha muhimu tusiwe is a wezi wa fadhila, and huyu mtu tumemuajiri na mpira ndio chanzo chake pekee cha kumpata riziki nae Ana Familia is a kwanini afanyishwe kazi bila ya kumpa haki yake hiyo ni fedheha kubwa lazima niseme ukweli na vipi mtu kama huyo atakuqa na morali?
ReplyDeleteKama issue ni kukosa kulipwa basi asinge cheza kabisa au asinge omba msamaha, kuomba msamaha maana yake amekiri lilikua kosa, mchezaji anatakiwa kuwa kioo cha jamii whatever the case kwa mchezaji smart hawezi kushindana na mashabiki kila mshabiki anaakili yake, lolote litakalo kutokea hakuna atakae kuelewa, mfamo wange mshambulia nani wa kulaumiwa? Au matusi waliomtukana anaweza kurudisha yote?
ReplyDelete