KOCHA na mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa ya
Ujerumani, Jurgen Klinsman amesema kuwa, anaamini mchezo wa hatua ya 16 bora ya
michuano ya Euro 2020 kati ya timu ya Taifa ya England dhidi ya Ujerumani,
utakuwa mchezo mgumu kutabilika kutokana na viwango vya timu hizo mbili kwa sasa.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa siku ya Jumanne ijayo katika
dimba la Wembley nchini England, ambapo Ujerumani wamefika katika hatua hiyo
baada ya kumaliza katika nafasi ya pili ya kundi F, nyuma ya Ufaransa.
Akizungumzia mchezo huo Klinsmann amesema: “Timu zote mbili
zinaonekana kuwa na ufanano kwa kiasi kikubwa hasa katika maeneo mengi, nadhani
utakuwa mchezo wenye uwiano sawa, na ambao hauwezi kutabirika”
0 COMMENTS:
Post a Comment