CLATOUS Chama, mtambo wa mabao ndani ya Simba amerejea ndani ya kikosi cha Simba baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na matatizo ya kifamilia.
Ndani ya Ligi Kuu Bara, Chama raia wa Zambia amehusika katika jumla ya mabao 20 kati ya 65 ambayo yamefungwa ndani ya mechi 28.
Chama alikuwa nchini Zambia baada ya mkewe Mercy Mukuka kutangulia mbele za haki, Mei 29 hivyo hakuwepo katika mechi zilizofuata ndani ya Simba.
Alikosekana katika mchezo dhidi ya Namungo 1-3 Simba, Mei 29, Ruvu Shooting 0-3 Simba, Juni 3 na Polisi Tanzania 0-1 Simba, Juni 19.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Simba waeandika kwamba Amerudi, triple C.
Pole kwake kwa msiba uliompata. Tunamwombea utulivu aendelee na majukumu yake
ReplyDeleteWelcome Mr chama l miss to much
ReplyDeleteKwanza pole sana kwa msimba ambao umetutikisa sote. I kurejea kwako kumewafanya wanaouota ubingwa wasijiweze kama ulivowaona wakichezeshwa kindumbwe ndubwe na waliokwishashuka daraja
ReplyDeleteKaribu saana chama na maisha lazima yaendelee
ReplyDeletePole sana kwa msiba mkubwa, lakini Mungu atakurejeshea amani Tunakupenda welcome mwamba wa Lusaka.
ReplyDelete