June 2, 2021

 


MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa kesho wanauhakika wa kuwapapasa wapinzani wao Simba iki kubadili wimbo kwa kila Mtanzania.


Ruvu Shooting itawakaribisha wapinzani wao Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Juni 3.


Katika mchezo wao wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru, ubao ulisoma Simba 0-1 Ruvu Shooting hivyo kesho wanahitaji kulinda rekodi yao na Simba wao wanawaza kulipa kisasi.


Masau amesema:"Hamna namna tunataka kuwafunga Simba ili kuonyesha kwamba nasi tupo imara, suala la wao kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika hiyo haitutishi tutafanya vizuri na tupo imara," .


Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara,  Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10 na pointi 37 huku Simba ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 64.

5 COMMENTS:

  1. Ndugu Masau Bwire, hivi katika ligi ya VP timu ya kuifunga ni Simba tu?

    ReplyDelete
  2. Nilikua namuona mtu wa maana tena mwalimu lakini kumbe ziro

    ReplyDelete
  3. Msiende na matokeo jamani mpira haupo hivyo eti.si simba wala ruvu msiende na matokeo.

    ReplyDelete
  4. Lakini basda ya matokeo mjitokeze kama mnavojitokeza Sasa na Wala msiingie mitini. Jitahidini kuifunga Yanga ambayo ndio kiasi chenu na Wala si is a Simba shujaa WA Afrika

    ReplyDelete
  5. Mechi ikiisha anaishia kusema tumefungwa na timu Bora africa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic