June 12, 2021




IMEELEZWA kuwa 
usajili wa beki wa kulia wa AS Vita, Shaban Djuma kuibuka ndani ya Yanga umeweka rekodi kwa kutumia gharama kubwa kumpata huku dau likiwa linakadiriwa kufikia Sh milioni 500.


Yanga imefanikisha usajili huo Jumatano ya wiki hii, Juni 9, baada ya Makamu wa Kamati ya Mashindano

na Usajili wa Yanga, Injinia Hersi Said kusafiri

kwenda nchini DR Congo kufanikisha usajili wa nyota huyo.


Timu hiyo ilikuwepo kwenye mipango ya muda mrefu ya kufanikisha usajili wa beki huyo ambaye inaelezwa klabu kubwa za TP Mazembe, Al Ahly na Mamelodi Sundowns zilikuwa zikiwania saini za nyota huyo.




Kabla ya Djuma wachezaji wengine waliokuwa wanaongoza katika usajili ghali ni Wakongomani Tuisila Kisila, Mukoko Tonombe ambao dau lao lilifikia Sh 250Mil wakitokea AS Vita, Mrundi Said Ntibazonkiza ‘Saido’ Sh 150Mil kwa upande wa Simba wapo Mzambia Clatous Chama Sh 300Mil na Luis Miquissone Sh 173.4Mil.


Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka kwa mmoja wa mabosi wakubwa wenye ushawishi wa timu hiyo, Yanga imefanikisha usajili huo kwa asilimia mia moja baada ya kufikia makubaliano mazuri na meneja wa Djuma.


Mtoa taarifa huyo alisema kuwa Djuma amesaini mkataba wa miaka miwili huku dau lake likitajwa kuwa si chini ya Sh 500Mil. Ni rekodi kubwa ya usajili ambayo haijawahi kutokea kwa mchezaji kuwahi kusajiliwa katika Ligi Kuu Bara.


Aliongeza kuwa, Injinia pia alikuwa katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa FC Lupopo, Ciel Ebengo Ikoko.


“Yanga tumepania hivi sasa katika usajili wetu na hiyo ni katika kutengeneza kikosi imara kitakachofanya vema katika michuano ya kimataifa ambayo mwakani tutashiriki,” alisema mtoa taarifa huyo.

8 COMMENTS:

  1. Ama kwwli sasa yanga wamkuwa matajiri kweli. Kwa usajili huo kama hamtochukuwa ubingwa msimu ujao mjuwe mmekwisha na waliokubebeni kuingia mitini

    ReplyDelete
  2. Una uchungu ww nguruwe fc kajifungue leba ya muleba

    ReplyDelete
  3. Luis ni million 700, rekodi yake haijavunjwa bado. Djuma shabani hata timu ya Taifa hajaitwa ujue Yanga bado hawajielewi

    ReplyDelete
  4. Tushawazoea wanasajili pesa kubwa na majina makubwa wanakuwa kuwalisha matembele na mihogo wanakuwa magalasa
    Wanaume tunabeba tu ndoo

    ReplyDelete
  5. Mambo ya Yanga wengine wanateseka

    ReplyDelete
  6. Bongo tatzo kweny usajil uku mbwembwe nying ukija kweny ligi kimeumana.,.,.duh ngoja tuone@#

    ReplyDelete
  7. Ila mkumbuke djuma alivunjika mguu msije mkasema mlikuwa hamjui

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic