IMEELEZWA kuwa Klabu ya Yanga imemalizana na nyota wa kikosi cha Mbeya City, Kibu Denis kwa kumpa dili la miaka miwili kuitumikia timu hiyo.
Kibu amekuwa kwenye kiwango katika mechi zake ndani ya Mbeya City ambayo inapambana kubaki ndani ya ligi.
Habari zimeeleza kuwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi imemalizana na nyota huyo ambaye mchezo wake wa kwanza akiwa na jezi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilikuwa Juni 13 mbele ya Malawi na alitumia dakika 25.
"Kibu kwa sasa anasubiri muda kutua Yanga kwani kila kitu kimekwenda sawa na kilichobaki ni suala la siku ya kutambulishwa," ilieleza taarifa hiyo.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa sasa usajili bado haujaanza hivyo wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.
Kwenye msimamo ikiwa nafasi ya 13 na pointi 36 baada ya kucheza mechi 31 msimu wa 2020/21.
Kesho Juni 22 ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Simba kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.
Tena?? C mlisema wameshamalizana .... Hahahaa
ReplyDeleteYaani hawa jamaa kwa habari za uongo wameshindikana....kila siku habari ni hiyo hiyo inageuzwa geuzwa tu
ReplyDeleteKwa namna ulivo mwenendo waSimba na yanga is a basi nahakikisha kuwa kabla ya kuanza msimu ujao basi Simba keshauchukuwa ubingwa huo kwasababu siku njema huanzia asubuhi na hizo kambi za kutoka Congo moja na kwenda yapilu hazitoleta isipokuwa magalasa tu
ReplyDelete