WAKATI leo kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi kikitarajiwa kushuka Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Biashara United nyota wake sita itawakosa.
Mchezo wa leo ni wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho na mshindi wa leo atacheza fainali na mshindi wa mchezo kati ya Azam FC na Simba utakaochezwa kesho, Uwanja wa Majimaji, Songea.
Nyota hao ni pamoja na Lamine Moro, Michael Sarpong, Metacha Mnata hawa kutokana na masuala ya nidhamu ndani ya kikosi hicho.
Mapinduzi Balama, Yassin Mustapha na Abdalah Shaibu, 'Ninja' hawa bado hawajawa fiti kutokana na kutibu majeraha yao.
Kwa mujibu wa Ofisa Uhamasihaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa Balama, Ninja maendeleo yao ni mazuri.
Wapo wanaofurahia kwa haya
ReplyDeleteBalama ameanza kuendelea vizur tangu msimu unaanza mpaka leo..... Mtafutieni tiba ya uhakika asije akapotea kwenye soka wkt dogo anakipaji Kikubwa
ReplyDeleteAnaendelea vizuri ni kutoka asilimia 30 kwenda 40 nk. Sio kutoka asilimia 30 kwenda 90 ndio maana muda umekuwa mrefu.
ReplyDelete