OBREY Chirwa, nyota wa kikosi cha Azam FC amesema kuwa suala la mkataba wake ndani ya kikosi hicho anawaachia mabosi zake kwa kuwa wao wanajua siku ambayo mkataba wake utameguka.
Chirwa ana uzoefu wa soka la Tanzania ambapo aliwahi kucheza kwa mafanikio ndani ya kikosi cha Yanga kisha akasepa na kuibukia nchini Misri.
Kwa sasa yupo ndani ya viunga vya Azam Complex inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina na kandarasi yake inakaribia kuisha msimu huu.
Nyota huyo amesema:"Kuhusu mkataba mimi ninawaachia viongozi siwezi kusema jambo lolote, ninawaachia mabosi wangu kwa kuwa wao wanajua kwamba mkataba wangu utaisha.
"Mimi nimecheza Tanzania na mzoefu hapa Tanzania, Mungu akijalia nitabaki na ikishindikana nitaondoka kwa kuwa timu zipo.
"Viongozi wananijua nimekaa miaka miwili hivyo ninajua kwamba wanajua nafasi yangu, wakinipa nafasi nitasajiliwa kama nafasi hapana nitasajiliwa timu nyingine," amesema.
Ndani ya Azam FC katika Ligi Kuu Bara, Chirwa ametengeneza jumla ya pasi nne za mabao na ametupia mabao matano.
0 COMMENTS:
Post a Comment