NYOTA wa Simba, kiungo Ibrahim Ajibu anapata tabu chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes kwa kujenga ushkaji mkubwa na benchi huku akishindwa kufikia rekodi yake ya msimu wa 2018/19 alipokuwa Yanga.
Nyota huyo alikuwa ni namba moja kwa kutengeneza pasi za mwisho Bongo, ambapo alitoa jumla ya pasi 17 ambazo hazijaweza kuvunjwa na nyota yoyote kwa sasa katika Ligi Kuu Bara.
Msimu huu akiwa ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ameshindwa kufurukuta kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba jambo ambalo limemfanya acheze jumla ya mechi 7.
Katika mechi hizo saba ni mechi tatu alianzia kikosi cha kwanza na nne akianzia benchi. Ametumia jumla ya dakika 236 akiwa ametupia bao moja na kutoa pasi moja ya bao.
Gomes amesema kuwa mchezaji atakayepata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza ni yule atakayefanya vizuri mazoezini.
Imekuwa ikitajwa kuwa nyota huyo msimu ujao atakuwa ndani ya kikosi chake cha zamani cha Yanga baada ya kupewa dili la miaka miwili.
Ikiwa dili hilo litakamilika atajiunga na timu hiyo bure kwa kuwa dili lake la miaka miwili linafika ukingoni msimu utakapomeguka.
Deal gani atafute timu nyingine yanga atumtaki
ReplyDeleteGlobal publishers seems virus infected
ReplyDeleteYes, it doesn't open
ReplyDeleteYanga ileee inarudi, huku ajibu kule makambo
ReplyDeleteHatumtaki katu!!! aende zake tu Ihefu au Gwambina
ReplyDeleteMna dharau sana, hamna shukurani ndio maana mnaitwa mnyama fc
ReplyDelete