June 20, 2021


KIKOSI cha Simba jana Juni 19 kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Shukrani kwa Luis Miquissone ambaye alifunga bao pekee la ushindi dakika ya 28 kwa pigo huru ambalo lilimshinda mlinda mlango wa Polisi Tanzania Mohamed Yussufu.

Ushindi huo unaifanya Simba kusepa na jumla ya pointi 6 mazima mbele ya Polisi Tanzania ambapo kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 2-0 Polisi Tanzania.

Licha ya Polisi Tanzania kupambana kusaka ushindi kwenye mchezo huo jitihada zao zilikwamia kwenye mikono ya kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula ambaye alitimiza majukumu yake kwa umakini.

Alikuwa ni Tariq Seif wa Polisi Tanzania alikosa nafasi ya wazi kumtungua Manula kwa pasi ya Daruesh Saliboko dakika ya 7 pia dakika ya 72 Gerad Mdamu alifanya jaribio kwa kichwa ndani ya 18 likaokolewa na Manula.

Mzee wa kukera Bernard Morrison alionekana amekasirika baada ya kukosa kucheza mchezo wa jana kwa kuwa alikuwa kwenye benchi na alinyanyuliwa kwa muda ili kufanya mazoezi ila hakuweza kuingia na alionekana akipigapiga chupa za maji.

Sasa Simba imefikisha jumla ya pointi 70 baada ya kucheza mechi 28 wamebakiza mechi mbili ambazo ni sawa na dakika 180 ikiwa watashinda zote basi watatangazwa kuwa mabingwa kwa kuwa watafikisha jumla ya pointi 73 ambazo hazitafikiwa na wapinzani wao Yanga na Azam FC.  ambao ni washindani wao wa karibu.

7 COMMENTS:

  1. Kwan siku hizi mechi moja ni point1

    ReplyDelete
  2. Ikifikisha point 73 hakuna timu itayofikisha pointi hizo kwahivo inahitaji mechi moja tu kwanini mbili na ikishinda mechi ijayo na Mbeya city tu kabla ya kucheza na yanga wa jadi. Hongera ya kutanguliza kwa Mnyama

    ReplyDelete
  3. Wivu na kutengeneza story ndo wamesowea

    ReplyDelete
  4. Mtunzeni mental fresh wenu..hahaha

    ReplyDelete
  5. Jamani hebu kuweni serious kidogo mnapoandika story, Simba akishinda mechi mbili atakuwa na point 73 toka 70? Pia Yanga ana 64 bado michezo 4 si aktafikisha 76 akishinda zote? Jamani Saleh Jembe wewe ni msomi , mwandishi wa habari, lakini blog yako story wanazotupa watu wako hapana

    ReplyDelete
  6. Baada ya mechi mbili itafikisha point 76 simba sio 73 mwandishii vingii unatudanganya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic