June 20, 2021

 


MABAO mawili ya kujifunga katika mchezo wa Euro 2020 ndani ya dakika nne yamewasaidia Ujerumani kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Ureno ndani ya kundi F.


Ni Cristiano Ronaldo alifungua pazia la mabao dakika ya 15 katika Uwanja wa Allianz Arena liliwekwa usawa na Alvez Dias aliyejifunga dakika ya 35 pia Raphael Guerrero alijifunga dakika ya 39.

Mpaka kipindi cha kwanza kinakamilika ubao ulikuwa unasoma Ureno 1-2 Ujerumani kasi iliendelea kipindi cha pili ambapo Kai Havertz aliongeza bao la tatu kwa Ujerumani dk ya 51 kisha msumari wa nne ulipachikwa dk 60 na Robin Gosens na bao la pili kwa Ureno lilipachikwa na Diogo Jota.

Ndani ya kundi F ni Ufaransa iliyolazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Hungary ipo nafasi ya kwanza na pointi 4 huku Ujerumani ikiwa nafasi ya pili na pointi 3 sawa na Ureno iliyo nafasi ya tatu huku Hungray ikiwa nafasi ya nne na pointi moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic