CRISTIANO Ronaldo ameonyesha umwamba wake kwa kutimiza majukumu yake kwenye timu ya taifa ya Ureno baada ya kusawazisha bao lililofungwa na wapinzani wao Ufaransa na kuwafanya watinge hatua ya 16 bora kwenye Euro 2020 wakiwa nafasi ya tatu.
Ronaldo alianza kupachika bao la kwanza dk 30 kwa mkwaju wa penalti likawekwa sawa na Karim Benzema wa Ufaransa dk 45+2 kwa mkwaju wa penalti na kufanya ubao wa Uwanja wa Puskas kusoma Ureno 1-1 Ufaransa kwa muda wa mapunziko.
Iliwachukua dakika mbili za kipindi cha pili Ufaransa kupachika bao la pili dk 47 kupitia kwa mfungaji wao yuleyule Benzema kwa pasi ya nyota Paul Pogba ambalo lilisawazishwa na Ronaldo dk 60 kwa mkwaju wa penalti na kumfanya afikishe jumla ya mabao 109 akifikia rekodi ya Ali Daei.
Kwenye kundi F ambalo lina timu nne ni Ufaransa inaongoza ikiwa na pointi tano na itacheza na Switzeland, Ujerumani ipo nafasi ya pili na pointi 4 itakutana na England na Ureno ambao ni mabingwa watetezi ipo nafasi ya tatu itakutana na Ubelgiji huku Hungry ikiwa nafasi ya nne imeishia hatua ya makundi.
Wafungaji wa mabao kwenye mchezo huo wote ni washkaji na waliwahi kucheza wote ndani ya Real Madrid kati ya msimu wa 2018/19.
0 COMMENTS:
Post a Comment