UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba kwa sasa unaendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi zao zote zilizobaki ikiwa ni pamoja na ule ujao dhidi ya Ruvu Shooting.
Yanga inanolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi raia wa Tunissia ambaye kwa sasa ameendelea kuwanoa vijana hao walio nafasi ya pili na pointi 61 kwenye msimamo.
Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa tayari wachezaji ambao hawana majukumu katika timu zao za taifa wapo kambini, Kigamboni kwa ajili ya mechi zao zilizobaki.
“Maandalizi kwa ajili ya mechi zetu ambazo zimebaki yameanza kwa kuwa wachezaji wapo kambini kwa sasa wakiendelea na mazoezi ili kuweza kupata matokeo chanya kwa kuwa malengo yetu ni kushinda mechi zetu zilizobaki,” alisema Bumbuli.
Mchezo wao ujao utakuwa ni Juni 17, Uwanja wa Mkapa ni dhidi ya Ruvu Shooting, mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 2-1 Ruvu Shooting.
Safari hii ubao utasema Ruvu 2 Matopolo 1
ReplyDeleteUnaota mchana!
DeleteNdio
ReplyDeleteNguruwe fc bwana hahaha
ReplyDelete