July 28, 2021

KAMA ulikuwa unahisi ni utani basi jua kuwa klabu ya Al Ahly wapo siriazi katika ishu ya usajili wa winga wa timu hiyo Luis Miquissone ambapo tayari klabu hiyo imewasilisha ofa ya pili ya Bilioni 2 za Kitanzania kwa mchezaji huyo huku mwenyewe Miquissone akikubali kujiunga na Al Ahly.

Al Ahly kwa muda mrefu wamekuwa wakitajwa kuiwania saini ya Luis Miquissone mwenye uraia wa Msumbiji ambaye tangu ajiunge na Simba Januari 2020, amekuwa kwenye kiwango bora kinachozifanya klabu mbalimbali kumuwania.

Luis Miquissone ameonyesha kiwango bora katika michezo yote miwili ambayo simba ilicheza dhidi ya Al Ahly katika ligi ya Mabingwa Afrika katika msimu uliopita ambapo alifanikiwa kuwafunga timu hiyo bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

Wakala mmoja wa wachezaji kutoka katika kampuni ya FMC  inafanya kazi na Luis, ambaye jina lake hakutaka kutajwa amesema kuwa Al Ahly imetuma ofa ya Bilioni 2 kwa Simba ambapo wiki hii wataanza kuijadili ofa hiyo kwa pande zote mbili, huku mchezaji mwenyewe akikubali kujiunga na Al Ahly baada ya kuuambia uongozi wake kuwa yupo tayari kujiunga na klabu hiyo.

“Klabu ya Al Ahly mara ya kwanza iliweka bilioni 1.6 ambazo zimeonekana kuwa ndogo kwa Simba lakini mara baada ya kutuma ofa ya bilioni 2 kwa uongozi wa Simba, umeonekana kukubali kukaa mezani na Al Ahly kwa aajili ya mazungumzo ambapo wiki hii watakutanba kujadili ofa hiyo.

“Kuhusu mchezaji mwenyewe yupo tayari kujiunga na Al Ahly, tayari ameuambia uongozi wake kuwa yupo tayari kujiunga na kocha wake Pitso Mosimane ambaye walifanya kazi wote katika klabu ya Mamelodi Sundwons,” Kimesema Chanzo hiko.

Alipotafutwa mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu juu ya ishu hiyo amesema kuwa “Kila kitu kuhusu masuala ya usajili wa wachezaji wa Simba watakaoingia, na watakaotoka ipo chini ya Mtendaji mkuu wa timu ambaye anahusika katika kutoa taarifa hizo.

4 COMMENTS:

  1. ila wasije wakatuma hyo pesa kwenye cm itakatwa yote na mchembaπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

    ReplyDelete
  2. Aruhusiwe atakuwa chachu ja balozi mzuri kwa simba. Watumie pesa hoyo kusajiri vijana wenye uchu wa mafanikio kama huyu, ndio mpira unavyofanya biashara.

    ReplyDelete
  3. Du haya nenda bhana kwa wanao chukua kombe la club bingwa afrika wengine mikia tu

    ReplyDelete
  4. Vzr sana... Ila akienda ajitaidi kugbania namba maaana na aly ahly sio watu wazurii

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic