July 28, 2021

BONDIA Mtanzania, Hassan Mwakinyo amefunguka kuwa kutajwa kama bondia namba moja kwa viwango vya ubora Afrika uzito wa Super Welter, ni deni kubwa sana kwake kuona anajituma kufanya vizuri zaidi.

Mwakinyo kupitia mtandao unaotunza takwimu za mabondia duniani ametajwa wa Boxrec ametajwa kuwa namba moja Afrika, na namba 37 Duniani kati ya Mabondia 2,050 kwenye uzani wa Super Welter.

Akizungumzia mafanikio hayo Mwakinyo amesema: “Namshukuru Mungu, na sapoti ya Watanzania wote bila kusahau uongozi wangu. Naamini kuwa namba moja Afrika sio kitu kidogo, hivyo nina deni kubwa la kuendelea kupambana kuongeza ubora wangu.”

Mabondia wengine wa Tanzania waliotajwa kwenye listi hiyo ni Kulwa Bushiri nafasi 21, na Nicholaus Michael Mdoe nafasi ya 22.

2 COMMENTS:

  1. Pambana uingie kwenye 10 ya dunia

    ReplyDelete
  2. N record nzur Sana ukilinganisha na muda alocheza na pia umri alonao bado mdogo anaweza fanya makubwa zaid

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic