July 10, 2021

 


UONGOZI wa kikosi cha Azam umeweka wazi kuwa bado unaendelea kusubiri ripoti ya kocha wao mkuu, George Lwandamina kwa ajili ya maboresho ya kikosi kupitia usajili, na usajili unaofanyika kwa sasa ni ule uliopendekezwa kabla ya dirisha dogo la usajili.

Azam mpaka sasa wamekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Cape Town City ya Afrika Kusini, Charles Zulu ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili utakaoanza rasmi msimu ujao wa 2021/22.

Pamoja na nyota huyo Azam itakayoshiriki michuano ya kimataifa msimu ujao imewaongezea mikataba baadhi ya wachezaji wao nyota wakiwemo Prince Dube, Idd Nado, Ayoub Lyanga na Bryson David.

Akizungumzia usajili huo, Mkuu wa Kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Unajua watu wengi wanadhani kuwa usajili tunaoufanya sasa unatokana na ripoti ya msimu huu ya kocha Lwandamina, lakini hapana nyota wote ambao wamesajiliwa mpaka sasa ni wale waliopendekezwa kabla ya dirisha dogo.

“Kuhusu ripoti mpya ya usajili bado tunaisubiri kutoka kwa kocha Lwandamina, na hii ataitoa mara baada ya kumalizika kwa ratiba ya michezo ya msimu huu.”

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic