MSHAMBULIAJI kinda wa kikosi cha
klabu ya Machester City na timu ya Taifa ya England, Phil Phoden yupo katika
hatari ya kuukosa mchezo wa fainali ya michuano ya Euro 2020, kufuatia majeraha
madogo aliyoyapata jana Ijumaa.
Kikosi cha England kimekamilisha
maandalizi yao kuelekea mchezo huo wa fainali, katika mazoezi yaliyofanyika
kwenye kituo cha mazoezi cha St George's.
Kikosi hicho cha kocha Gareth
Southgate kina nafasi ya kumaliza ukame wa muda mrerfu wa kushinda kombe katika
michuano mikubwa wakicheza kwenye ardhi yao ya nyumbani, ambapo mara ya mwisho
kufanya hivyo ni katika michuano ya kombe la dunia ya mwaka 1996.
Nyota wote 25 walikuwa sehemu ya
mazoezi hayo ya mwisho ya England, huku Foden akiwa ndiye nyota pekee
akliyepumzishwa. Uamuzi wa kumuondoa Foden katika mazoezi hayo ya mwisho
ulifanywa na madaktari wa kikosi hicho jana Ijumaa.
0 COMMENTS:
Post a Comment