TIMU ya Taifa ya Brazil kesho Julai 6 inaanza rasmi kusaka ubingwa wake wa 10 wa Copa America na itavaana na wabishi Peru katika hatua ya nusu fainali.
Brazil mwaka huu wamekuwa na mwendo mzuri ambapo waliweza kufika hatua hiyo baada ya kuibuka na ushindi mbele ya Chile kwa ushindi wa bao 1-0 katika hatua robo fainali.
Mchezo huo ulikuwa ni mgumu kwa Brazil na ilicheza ikiwa pungufu baada ya nyota wao Gabriel Jesus kuonyeshwa kadi nyekundu.
Timu hiyo ambaye ina mshambuliaji mwenye majivuni mengi, Neymar Jr inatakiwa kupambana kupata ushindi ili iweze kutinga hatua ya fainali.
0 COMMENTS:
Post a Comment