July 5, 2021


KIKOSI cha Simba ambacho kinatetea mataji mawili kwa sasa kwenye ardhi ya Bongo kina vigongo vya moto kukamilisha mipango yao kwa msimu wa 2020/21.

Kwa sasa kikiwa kina kazi ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara kina pointi 73 nafasi ya kwanza na ni mechi nne mkononi zimebaki wakiwa wanahitaji pointi tatu kutangazwa kuwa mabingwa.

Hivi hapa vigongo vyake:-

KMC  v Simba, Uwanja wa Mkapa, Julai 7.

Simba v Coastal Union, Uwanja wa Mkapa, Julai 11

Azam v Simba, Julai 14, Uwanja wa Azam Complex.

Simba v Namungo, Julai 18, Uwanja wa Mkapa.


Kwa upande wa taji la Kombe la Shirikisho pia Simba ni mabingwa watetezi wana kibarua dhidi ya Yanga, huko Kigoma.

 Itakuwa namna hii:-Simba v Yanga, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, huu ni wa Kombe la Shirikisho, hatua ya fainali.

Kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula amesema kuwa bado wana kazi ya kuweza kupambana ili kuonyesha ukubwa wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes.

1 COMMENTS:

  1. Hakuna cha vigongo wala nini, makombe yote mnyama anabeba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic