July 1, 2021

 


PRINCE Dube nyota wa kikosi cha Azam FC kuna hatihati ya kuikosa tuzo ya mfungaji bora kutokana  na kusumbuliwa na tatizo la tumbo.

Nyota huyo raia wa Zimbabwe ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Azam FC akiwa ametupia mabao 14 sawa  na John Bocco wa Simba ambaye anapewa nafasi ya kuipoka tuzo hiyo.

Mtetezi wa tuzo hiyo ni Meddie Kagere mwenye mabao 11 naye bado anapewa nafasi ya kuweza kusepa na tuzo hiyo kwa kuwa bado Simba ina mechi mkononi.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa nyota huyo amefanyiwa vipimo mara tatu ila katika hali ya kushangaza tatizo limekuwa likijirudia.

"Dube yupo vizuri kwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na tumbo ilitokea ghafla kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rhino Rangers.

"Tumemfanyia vipimo mara tatu huku hali ikionekana kuwa yupo sawa lakini tatizo hilo limekuwa likijirudiarudia jambo ambalo linamfanya awe nje ya uwanja," .

Kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba aliweza kuwa benchi na kushuhudia timu yake ikifungwa bao 1-0.

Ilikuwa Uwanja wa Majimaji, Songea na bao la ushindi lilifungwa na Luis Miquissone kwa pasi ya Bernard Morrison.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic