July 1, 2021


GEORGE Mketo, Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania amesema kuwa ushirikiano ambao wanaonyesha wachezaji ndani ya uwanja unawapa nguvu ya kufanya vizuri kwenye mechi zao ambazo zimebaki.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 32 imekusanya pointi 42 kwenye msimamo ipo nafasi ya 7 huku kinara akiwa ni Simba mwenye pointi 73.

Kocha huyo amesema kuwa kila mchezaji anatimiza majukumu yake ndani ya uwanja jambo ambalo linawafanya wawe na imani ya kupata matokeo kwenye mechi zao ambazo zimebaki.

"Kila mchezaji anapambana ili kupata pointi tatu ni lazima kila mmoja apambane ili kuona timu inashinda na kwa namna ambavyo wachezaji wanafanya kwetu ni furaha.

"Tunajua kwamba ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi na ni jambo zuri kwa sababu ili kuwa na timu imara lazima ipate ushindani kutoka kwa wengine hilo halitupi tabu," .

Miongoni mwa wachezaji wakongwe ndani ya Polisi Tanzania ni pamoja na beki kisiki, Kelvin Yondan ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Malale Hamsini.

Yondani alijiunga na Polisi Tanzania akiwa ni mchezaji huru baada ya mabosi wake wa Yanga kuachana naye msimu uliopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic