July 18, 2021


KIUNGO mchezeshaji kipenzi cha Yanga, Salum Abdallah ‘Fei Toto’, hana hofu na mchezo wa

fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports

(ASFC), maarufu kama FA watakaocheza dhidi ya Simba kwani hizo ndiyo mechi zake anazotamani kuzicheza.


Kauli hiyo huenda ikawa salamu kwa viungo wa Simba atakaokutana nao tena katika mchezo huo ambao ni Luis Miquissone, Clatous Chama,Larry Bwalya na Taddeo Lwanga atakaokutana nao.


Timu hizo zinatarajiwa kukutana kwa mara ya pili katika mchezo huo wa fainali utakaopigwa Julai 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika wa mkoani Kigoma.


Akizungumza na Championi Ijumaa, Fei Toto alisema kuwa kwake michezo yote dhidi ya Simba ni miepesi kwake na anaichukulia kawaida tofauti na akikutana na timu ndogo.


Fei Toto alisema katika michezo yote iliyopita dhidi ya Simba alicheza chini ya presha kutokana na kufahamu uwezo wa kila mchezaji.


Aliongeza kuwa michezo dhidi ya timu ndogo inampa ugumu kutokana na kutowajua wachezaji wa timu pinzani. Hivyo ni katika kuelekea fainali ya FA, hana hofu ya mchezo na wataingia uwanjani kwa ajili ya kupata matokeo mazuri ya ushindi pekee.


“Mechi hizi za Kariakoo Dabi, mashabiki ndiyo wanaifanya kuwa ngumu kutokana na presha kubwa wanazokuwa nazo kabla ya mchezo husika.


“Kama wachezaji nikiwemo mimi mwenyewe sijawahi kuona ugumu wowote wa Kariakoo Dabi, ninacheza bila ya presha yoyote huku nikitimiza majukumu yangu ya uwanjani kuchezesha timu, kutengeneza mabao na kuzuia mashambulizi.


“Binafsi hizi ndogo ndiyo zinanipaga ugumu kila tunapokutana nazo uwanjani, kwani wachezaji wao wengi hatuwafahamu, hivyo wanatupa ugumu katika kupata matokeo,” alisema Fei Toto.

15 COMMENTS:

  1. Yeye ana jipya lipi hasa? Afunge bakuli lake acheze hayo makida makida, k8la siku kidomodomo tuu

    ReplyDelete
  2. Ifike mahali wachezaji wajofunze kuheshimu timu zingine, haipendezi wewe kila kukicha unapngea maneno kuhusu timu zingine tujifunze kwa wenzetu. Huwezi kumsikia mchezaji wa man u au chelsea anazungumzia timu ya man city au liver, never.

    ReplyDelete
  3. Ulimi hauna mfupa. Wewe ni mchezaji safi lakini huenda hauna habari kuwa ni jana usiku tu Al Ahli imetwaa ubingwa kwa mara ya 11 na kwa msimuu huu Al Ahli Haijawahi kufungwa na timu yeyote isipokuwa na Simba tu ambayo unaielezea kuwa ni timu nyepesi kuifunga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tahadhari kuntu kabisa kwa Fei Toto. Akumbuke ulimi ulikiponza kichwa!!!!

      Delete
    2. Nadhani una tatizo la kumbukumbu mkuu

      Delete
    3. ....na hiyo Simba imefungwa na Yanga,JKT na Prisons.

      Delete
    4. Hii Simba mara zote imeidharau Yanga, lkn katika michezo Minnesota haijapata matokeo chanya. Na mechi ya mwisho ilifungwa kwa assist ya Fei Toto. Hii ina maana anachokisema ndicho tayari ameshakifanya

      Delete
    5. Kwa wepesi wa Simba anaousema Fei kumbe ndiyo sababu Yanga ndiyo mabingwa?

      Delete
  4. Hawachezi kwa malengo Ila wanacheza kwa sifa. Ndo maana ubingwa wanausikia tu

    ReplyDelete
  5. Wameotea moja basi maneno meeeengi

    ReplyDelete
  6. Wamechukua mara 27 we mara21 halafu unasema hawachukui makombe chukua mara tano zaidi tuone kama umemfikia yanga

    ReplyDelete
  7. Mwacheni aongee kashawafunga midomo yenu maana mlikua mnaongea sana

    ReplyDelete
  8. Ameisaidia timu yake kupata nn

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic