KIUNGO mshambuliaji wa Wydad Casablanca ya nchini Morocco, Simon Msuva, ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kubeba ubingwa wa ligi nchini humo, maarufu kwa jina la Botola Pro.
Nyota huyo amesema kuwa ilikuwa ni malengo yake kuona kwamba anaweza kutwaa ubingwa na timu hiyo.
Casablanca ilitangaza ubingwa huo baada ya kufanikiwa kuwafunga wapinzani wao Mouloudia Oujda mabao 2-0.
Msuva anaipa ubingwa huo Casablanca ukiwa ni msimu wake wa kwanza tangu ajiunge nao akitokea Difaa El Jadida ya nchini humo.
Ubingwa huo ni wa 21 ambao wameuchukua timu hiyo ambayo ilishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika pia msimu huu.
Kiungo huyo ameweka rekodi kubwa ambayo
baadhi ya wachezaji waliowahi kucheza na
wanaocheza akiwemo Nickson Kibabage
anayeichezea Club Athletic Youssoufia
Berrechid ya nchini humo, wamempongeza.
Akizungumzia ubingwa huo, Msuva alisema: “Ni
furaha kwangu kuweka historia yangu katika
maisha ya soka kuchukua ubingwa hapa
Morocco.
“Tangu najiunga na Casablanca haya yalikuwa
malengo yangu ya kwanza kubeba ubingwa wa
ligi kuu, licha ya kutamani zaidi kutwaa ubingwa
wa Ligi ya Mabingwa Afrika.”
0 COMMENTS:
Post a Comment