July 17, 2021

KOCHA mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes amefunguka kuwa baada ya kumaliza kibarua chao cha mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo, wameandaa programu ya siku saba za maandalizi ya mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga utakaopigwa Julai 25, mwaka huu.

Simba ambao tayari wametangazwa mabingwa wa Ligi Kuu kwa msimu wa nne mfululizo ambapo mpaka sasa wanaongoza msimamo na pointi zao 80 walizokusanya katika michezo 33 waliyocheza mpaka sasa.

Kesho Jumapili wanatarajiwa kukabidhiwa rasmi kombe lao kwenye sherehe zitakazofanyika kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Baada ya mchezo huo Simba wanatarajiwa kuwa na mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho utakaochezwa Julai 25, mwaka huu kwenye uwanja wa Lake Tanganganyika mkoani Kigoma.

Akizungumzia mipango yao, Gomes amesema: “Hatukucheza vizuri mchezo wetu uliopita wa ligi dhidi ya Azam, lakini baada ya hapa tutakuwa na mchezo wa kufungia msimu dhidi ya Namungo ambao tutajipanga kufanya vizuri.

"Baada ya hapo tutakuwa na maandalizi ya wiki moja kwa ajili ya mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga Julai 25, mchezo ambao ndilo lengo letu kubwa zaidi.”

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic