BAADA ya kujihakikishia nafasi ya kumaliza katika nafasi nne bora kwenye msimamo, na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao, Uongozi wa klabu ya Biashara United umetamba kuwa umejipanga vizuri na unakwenda kushindana kwenye michuano hiyo na si kushiriki.
Biashara United imepata tiketi hiyo rasmi juzi Alhamisi baada ya kupata sare ya bao 1-1 katika mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons. Sare hiyo imewafanya Biashara wafikishe pointi 50 walizokusanya katika michezo 33 waliyocheza mpaka sasa.
Akizungumzia malengo yao, Katibu mkuu wa Biashara United, Haji Mtete amesema: “Kwanza
tumefurahi kwa kufanikiwa kupata nafasi hii ya kuiwakilisha nchi katika
michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, tumejifunza mengi kutoka kwa
watangulizi wetu na hilo limetufanya tuanze maandalizi mapema.
“Tunajua ili kufanya vizuri kimataifa, tunahitaji kuwa na wachezaji bora na kuanza maandalizi mapema, hivyo tayari kocha wetu amefanya tathimini na kutoa mapendekezo ya wachezaji ambao tunapaswa kuwasajili ili kufanya vizuri katika michuano hiyo. Malengo yetu ni kushindana na si kushiriki.”
0 COMMENTS:
Post a Comment