BAADA ya Simba SC kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo katika Kombe la FA, huku wakiitawala Ligi Kuu kwa kutwaa makombe kwa misimu manne mfululizo, Mjumbe wa Bodi ya Utendaji ya Simba Zakaria Hans Pope ameibuka na kusema kuwa sasa mipango yao yote ni kuchukua ubingwa katika michezo ya kimataifa.
Simba imefanikiwa kufikisha idadi ya ubingwa mara nne mfululizo katika Ligi Kuu Bara hadi sasa pia imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Shirikisho la Azam mara tatu.
Akizungumzia mipango yao, Hans Pope amesema kuwa kwa ubingwa walionao sasa unatosha kudhidirisha kuwa wao ndio mabingwa wa nchi, na wanahitaji kupata ubingwa huo hata katika michezo ya kimataifa.
“Simba ni timu kubwa kwa sasa na ndio mabingwa wa nchi kwa kuwa tumeshachukua makombe ya Ligi Kuu mara nne, na sasa tumechukua Kombe la FA kwa mara ya tatu tayari inatosha kuonyesha ukubwa wetu.
“Tunachokitaka kwa sasa ni kuvuka
mipaka na kuchukua ubingwa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa
tumeshachukua sana huku nyumbani, na tumezoea ubingwa wa nyumbani hivyo kwa sasa
ni levo nyingine za kimataifa na kuonyesha ukubwa wa Simba,”amesema Hans Pope.
Baada ya manara sasa pip nae kawa msemaji wa timu
ReplyDeleteTimu ipi? Timu ya Familia? Wapenzi wa Mikia aka vichupi FC mchokezeni Barbra mwone kama hamtatimuliwa wote mrudi pale kwenye jengo lenu msimbazi mkauze vijana.
DeleteMkauze vijora
DeleteHahahahahahaaaaa
ReplyDeleteAngeongea mwingine lkn huyu???????
ReplyDeleteHanspooe ni Simba Damu mwengine yote semeni. Miongoni mwa wanasimba wanaoishi katika vipindi vya Raha na ziki na kamwe hatujamsikia na kauli za kutetereka juu ya mapenzi yake zidi ya simba. Ni mtu wa kujitoa kwa ajili ya Simba pia. Yanga kitu kinachowayumbisha kwa Muda Sasa ni kukosa watu Kama akina Hanspooe ndani Yanga.Kwa bahati nzuri Simba wamebahatika kuwa na hawa watu na wanasimba wanatakiwa kuwaenzi na kutambua mchango wao ndani ya simba. Watu kama Salum Abdalla try again,Akina Magori, akina Nghambi,akina kassim Dewji na wengine kadhaa nyuma ya pazia bila ya kmsahau mtendaji mkuu wa bodi ya wakurugenzi na Muekezaji Mohammed Dewji. Kuwepo watu kama akina Magori ndio bila Shaka waliowezesha kumshawishi Mo kuekeza ndani ya Simba kwa hivyo utaona umuhimu wa watu fulani katika muunganiko wa Mambo.Na hizi jitihada zao sio kwa ajili ya Simba tu bali nchi yetu kwa ujumla. Klabu zetu zikiwa zitaendelea kufanya vizuri basi hata wauza magazeti mitaani watafanya vizuri pia na media industry kwa jumla,tuamke katika kujenga vilivyo bora na kuwatia moyo wale wanaopambana katika maboresho.
ReplyDeleteMzee wa miundombinu......akizidi kumnanga Manara atajikuta anaanikwa maovu yake na mwendazake maana anajua yote aliyokuwa anayafanya yeye na Kaburu
ReplyDeleteSimba kamili gado
ReplyDeleteUyu ni mmoja ya viongoz walioinjinia usajili wa Morrison kwa kuwaingiza chaka wenzake sasa ngoja tuone kitachofata
ReplyDeleteSimba timu bora zaidi kutokea Africa
DeleteUtopolo mtasubiri sana
DeleteKwa suala la Morrison mtasubiri sana
ReplyDeleteMkwanja wetu wa nguvu tuautaka! Mtaona faida ya ukanjanja wake
DeleteHukumu ni kesho
ReplyDeleteSawa uncle kasepa ila kuwahi waungwana basi mpeni walao kiinua mgongo maana kaitumikia simba kwa nguvu zote
ReplyDeleteAkishalipwa Hamis Tambwe tutafanya hivyo
DeleteMsimu uhao Wataishia kwenye makundi kama walivyotolewa na UD Songo
ReplyDeleteWakishatplewa mapema waseme next level pia, wasijikaushe, hapo ndio tambo za Manara Vs Wadosi mtaziona
ReplyDeleteHata huko baada ya kugaragazwa mapema watayafanya yale yale ya ubabe kusema refa kawaonea na kupiga kupiga ngumi kama vile walipompiga Bocco wanapoona wameelemewa halafu kufunguwa kesi fifa kwakujiona wao majabari hawaogopi chochote. Ama kwa matusi Mungu awazidishie
ReplyDeleteAiseee machupi fc
ReplyDelete