NYOTA Francis Kazadi Kasengu amesema kuwa Mukoko Tonombe ni moja kati ya watu wanaomshawishi kwa kiasi kikubwa kujiunga na klabu ya Yanga kwa ajili ya msimu ujao.
Kazadi Kasengu na Mukoko Tonombe wamewahi kucheza kwa pamoja katika kikosi cha AS Vita lakini kwa sasa wanacheza kwa pamoja katika kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kazadi alisema kuwa amekuwa Akizungumza mara kwa mara na rafiki yake Mukoko Tonombe ambaye amekuwa akimuuliza kuhusu ligi ya Tanzania hususani kuhusu Yanga huku akiweka wazi kuwa kiungo huyo kamshawishi ajiunge na klabu hiyo.
“Mukoko ni rafiki yangu sana, tumecheza wote katika klabu ya AS Vita na timu ya taifa ya DR Congo, mara nyingi tumekuwa tukizungumza vitu mbalimbali haswa soka la Tanzania.
“Yeye ameniambia anatamani kuniona nikijiunga na Yanga, tulipokutana katika mechi ya timu ya Taifa aliniletea jezi ya Yanga hivyo ninayo jezi ya Yanga na siku zote ananishauri tucheze wote ndani ya Yanga.
“Mimi nipo tayari kujiunga na Yanga lakni sitaki kusema nini kinaendelea kwa sasa kwani kila kitu kitakuwa wazi hivi karibuni,”alisema mshambuliaji huyo.
Hivi msimu ujao kutakuwa na wacongo wangapi ndani ya yanga?
ReplyDeleteNini Wacongo hata wakija Wasomali au Wahindi tunachojali ni kurudisha heshima.Ila waambieni wale jamaa zenu pale TFF wasilete figisu figisu za kuunguza idadi ya wachezaji wa kigeni na pia kuweka masharti ya idadi ya wachezaji wa kigeni wanaopaswa kucheza kwenye mechi moja maana tumesikia wameshaanza kujadiliana jinsi ya kupiga spana ili mradi kuipiga brake Yanga
Deletekuunguza=kupunguza
DeleteHaikuhusu, ili mradi tubebe makombe
ReplyDeleteMsimu ujao kutakuwa na wacongo 11 kwenye first eleven ya Yanga. Na hakuna shida....
ReplyDeleteAs Vita iliyofeli inahamia bongo
ReplyDeleteWe acha kudanganya watu,sheria ikitungwa itahusu vilabu vyote siyo kubagua vingine.
ReplyDelete