July 27, 2021

 


BAADA ya Yanga kukamilisha usajili wa mshambulaiji wa AS Vita, Fiston Mayele, kocha msaidizi wa AS Vita Roul Shungu amesema kuwa Yanga imefanikiwa kumpata mshambuliaji mzuri atayekwenda kuwasaidia kufunga mabao ya kutosha katika safu ya ushambuliaji msimu ujao.


Shungu aliwahi kuwa kocha mkuu wa Yanga 
kuanzia mwaka 1998- 2001 na kufanikiwa kuipatia ubingwa wa ligi kuu katika msimu wa mwaka 1999/2000.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu moja kwa moja kutoka DR Congo, Shungu alisema kuwa Fiston Mayele ni moja kati ya washambuliaji bora wanaopatikana kwa sasa nchini Congo huku akisema kuwa njaa yake ya kufunga imekuwa ikimsaidia kufanya vizuri jambo ambalo anaamini pia atalifanya na kwa Yanga pia.

“Mayele ni mshambualiaji mzuri sana, kwa hapa Congo ni moja kati ya washambuliaji bora,utaona hata katika michuano ya CHAN yeye ndiye alikuwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya DR Congo na hata katika Klabu ya AS Vita yeye ndiye kinara wa kufunga katika msimu uliopita ndani ya timu.

 

“Hivyo hata Yanga huko anapokwenda naamini atafanya vizuri sana kwa kuwa ni mchezaji anayejua kufunga na ana njaa ya kufunga, kwetu sisi tunamtakia kila la kheri huko anapoenda na huo ndio maana ya mpira,” alisema kocha huyo.

16 COMMENTS:

  1. Mnahangaika sana kufuatilia usajili wa Yanga lakini Yanga wao wako kimya tu

    ReplyDelete
  2. Utafuatilia kipi kwa yanga tofauti na usajili maana hawana jipya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa kama hakuna jipya unacoment nini coment kwa wenye jipya

      Delete
    2. Mwambie huyo kiyazi apite mbali aachane na yanga

      Delete
  3. Vita alitolewa hatua ya makundi club bingwa na mayele alikuwepo lakini

    ReplyDelete
  4. Wacongo na warindi wanajua sana kupigiana debe

    ReplyDelete
  5. Usajili uwe wa uhakika tu msije mkatuletea ya mgiriki asie julikana tunataka majembe ya kupambana na kuirudishia yanga hadhi yake

    ReplyDelete
  6. Mashabiki wa simba mna hofu sana na Yanga fanyeni yenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unajidanganya

      Delete
    2. Wewe ushafanya yako??mungu akupe nguvu uweze kutafuta ada za watoto maana mama anaucheza mwingi,gari limepata dereva mla mirungi na pariki kuanzia mwakani utalipa ada za watoto.

      Delete
  7. Kama ni Mayele huyu huyu, nawahurumia. Afadhali Kisinda anasaidia DAKIKA 45 tu

    ReplyDelete
  8. Unashangaa vita kutolewa makundi hujuwi mpila fatilia ulaya ndio utajuwa mpila

    ReplyDelete
  9. mbona mikia mlitolewa na kaizer na chama alikuwemo ndani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic