BAADA ya Ujerumani kutupwa nje kwenye michuano ya Euro 2020 kufuatia kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Uingereza katika hatua ya 16 bora, kocha wa Timu ya Taifa ya Ujerumani, Joakim Low ameachia ngazi.
Kocha huyo ameomba msamaha pia kwa mashabiki kwa kushindwa kuwapa kile ambacho walitarajia kwa kuwa timu hiyo ilikuwa na nafasi ya kufanya vizuri ndani ya Euro 2020.
Kocha Low ameiongoza timu hiyo kwa miaka 15 na kufanikiwa kutwaa Kombe la Dunia 2014.
Baada ya kuachia ngazi kocha huyo amesema: “Imekuwa miaka 15 mirefu na yenye wakati mzuri sana, kwa kweli, lakini kuna baadhi ni ya kukatisha tamaa.
“Timu na wachezaji wana hatma nzuri mbele yao. Bahati nzuri kwa Hansi Flick (kocha mpya), namtakia kila la heri, moyo wangu unaendelea kudunda kwenye rangi nyeusi, nyekundu na dhahabu," .
0 COMMENTS:
Post a Comment