July 17, 2021

ALIYEKUWA kocha msaidizi wa kikosi cha klabu ya Simba raia wa Burundi, Masoud Djuma amesaini mkataba wa miaka miwili ndani ya kikosi cha Rayon Sports inayoshiriki Ligi Kuu nchini Rwanda. 

Djuma alijiunga na Simba mwaka 2017 na kuondoka Oktoba mwaka 2018, kutokana na kuwa na changamoto za mahusiano mabaya kati yake na kocha mkuu wa Simba wa wakati huo, Patrick Aussems.

Akiwa na Simba Djuma aliiongoza Simba katika mashindano ya Sportpesa mwaka 2018, ambapo Simba walimaliza kama washindi wa pili.

Taarifa rasmi ya klabu ya Rayon Sports kupitia mitandao yao ya kijamii imeeleza: “Tunayo furaha kutangaza kuwa tumefikia makubaliano na mchezaji wetu nguli, na nyota wa zamani wa kimataifa wa Burundi, Masudi Djuma Irambona.

“Djuma atakuwa kocha mkuu mpya wa klabu baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili, na anatarajiwa kuanza kutumikia majukumu yake mapya kuanzia msimu ujao wa 2021/22.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic