SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa leo pia Julai 7 kocha wa makipa Milton Nienov hatakuwepo kwenye benchi la ufundi baada ya kusepa Bongo.
Kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa leo Julai 7 kina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya KMC, Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.
Kocha Nienov raia wa Brazil, Julai 3 hakuwepo kwenye benchi la ufundi na mikoba yake alikuwa nayo kipa namba moja Aishi Manula ambaye alianza kikosi cha kwanza na mshikaji wake Beno Kakolanya alikuwa benchi.
Ilikuwa ni kwenye mchezo wa Kariakoo Derby baada ya dk 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga huku bao la ushindi likipachikwa na Zawad Mauya.
Kwa mujibu wa Matola amesema kuwa kocha huyo anasoma hivyo kipindi hiki ni cha mitihani.
"Kwa sasa kocha wa makipa hayupo na timu kwa sababu anasoma na wakati huu ni muda wa mitihani kwake hivyo akikamilisha masuala hayo atarudi.
"Kwenye mchezo wetu dhidi ya KMC pia atakosekana kama ambavyo alikosekana kwenye mchezo wetu uliopita," .
Mmmh xaw
ReplyDelete