July 7, 2021

 


ITAKUWA ni fainali kati ya Lionel Messi wa timu ya taifa ya Argentina dhidi ya Neymer wa timu ya Brazil kwenye Copa America, Jumamosi, Uwanja wa Maracana.

Argentina imeshinda hatua ya nusu fainali mbele ya Colombia kwa penalti 3-2 baada ya kipa Emiliano Martinez kuokoa penalti tatu. Muda wa kawaida ubao wa Uwanja wa Mane Garrincha ulisoma Argentina 1-1 Colombia.

Watupiaji wa mabao hayo walikuwa ni Lautaro Martinez dk 7 na liliwekwa usawa na Luis Diaz dk 61 kwa upande wa Colombia.

Ikumbukwe kuwa Argentina haijashinda taji hilo tangu ilipofanya hivyo 1993 itakutana na Brazil ambayo ilishinda hatua ya nusu fainali dhidi ya Peru Jumatatu kwa bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic