July 7, 2021


 TAARIFA za kuaminika kutoka ndani ya Yanga, zinadai kuwa viongozi wa timu hiyo wamepanga kumuongezea mkataba kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabi.

Uamuzi huo umekuja baada ya kuridhishwa na mwenendo wa timu hiyo tangu Nabi apewe jukumu la kuinoa kutoka kwenye mikono ya Cedric Kaze, huku pia akitoka kuifunga Simba.

Julai 3, Nabi alishuhudia wachezaji wake wakisepa na pointi tatu mbele ya Yanga kwa ushindi wa bao 1-0 Uwanja wa Mkapa jambo ambalo limewafurahisha mabosi wake.

Chanzo kutoka ndani ya Yanga, kimeliambia Spoti Xtra kuwa: “Viongozi wetu wa Yanga na wale wa GSM wameridhishwa na uwezo wa Nabi, ukiangalia amekaa muda mfupi tu lakini kuna mabadiliko makubwa sana yameonekana kwenye timu, hivyo wameanza kujadili suala la kumuongezea mkataba ili aijenge timu zaidi," .

Spoti Xtra lilimtafuta Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabit Kandoro kuzungumzia hilo, alisema:“Kiukweli Nabi alikuwa chaguo letu na ndiyo maana tulimpa kazi kwa sababu tulitambua ni mtu wa namna gani.

“Kuhusu kuibadilisha Yanga ni kweli kafanya hivyo. Lakini kuhusu mkataba mpya ni mapema sana kuzungumzia.”

Nabi alitua Yanga Aprili mwaka huu na kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu. Amefanikiwa kuiongoza timu hiyo kwenye michezo sita ya ligi, ameshinda minne, sare moja na kupoteza moja.

4 COMMENTS:

  1. Naona hapo waliotajwa ni viongozi wa Yanga tu na alieshangiliwa sana Manji hakutajwa wala katika mechi ya watani pia hakutajwa na wala hatusikii kutajwa ni vipi tena, hebu tupozeni kidogo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic