UONGOZI wa KMC umeweka wazi kwamba nahodha wao na kipa namba moja Juma Kaseja huwa anakuwa mwalimu akiwa kambini na muda wa mechi pia amekuwa akitoa hamasa kwa wachezaji wa timu hiyo.
Leo KMC inatarajiwa kumenyana na Simba kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa majira ya saa 1:00 usiku.
Akizungumza leo mapema na Global TV kupitia kipindi cha Krosi Dongo, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa Kaseja amekuwa ni chachu ya mafanikio ya timu hiyo kwa kuwafundisha wachezaji wao.
"Kaseja amekuwa ni mwalimu kwa wachezaji wenzake na pia wakati wa mechi amekuwa akiwapa hamasa wachezaji ili waweze kufanya vizuri.
"Uzoefu wake wa katika masuala ya mpira hasa akiwa amecheza kwenye mechi za ushindani muda mrefu zinamfanya awe imara na tunaamini kwamba yeye ni moja ya wachezaji muhimu katika kikosi cha KMC," .
Kaseja amecheza pia ndani ya Yanga na Simba kwa nyakati tofauti pia alikuwa ndani ya Kagera Sugar kwa nyakati tofauti.
0 COMMENTS:
Post a Comment