MSHAMBULIAJI namba tatu kwa utupiaji ndani ya Klabu ya Simba, Meddie Kagere ametupia bao lake la 12 baada ya kupitisha jumla ya siku 91 bila ya kufunga.
Namba moja kwa utupiaji kwenye kikosi cha Simba ni John Bocco mwenye mabao 15 anafuatiwa na Chris Mugalu mwenye mabao 13 kwa msimu wa 2020/21 ambapo Simba ni mabingwa wa ligi.
Mara ya mwisho nyota huyo kufunga ilikuwa ni Aprili 14 Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikishinda mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na alitupia mabao mawili kwa miguu yote miwili ule wa kulia pamoja na wa kushoto.
Nyota huyo aliweza kuyeyusha siku 91 ambazo ni sawa na saa 2,184 bila ya kufunga ndani ya Ligi Kuu Bara licha ya Simba kupata nafasi ya kucheza mechi za ligi ilikuwa dhidi ya Mwadui FC, Kagera Sugar,Gwambina,Dodoma Jiji,Namungo, Ruvu Shooting,Polisi Tanzania, Mbeya City,Yanga, KMC na Coastal Union.
Nyota huyo aliibukia Uwanja wa Azam Complex, Julai 15 zikiwa zimepita siku 91 na kuweza kufunga bao mbele ya Azam FC na timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Amekwisha ngoja amalizie mkataba wake
ReplyDelete