BEKI wa zamani wa klabu ya
Manchester City na timu ya Taifa ya England, Micah Richards amewataadharisha
nyota wa timu ya Taifa ya England kuwa makini katika mchezo wao wa fainali
dhidi ya Italy.
Richards ambaye amewahi kufanya
kazi chini ya kocha wa sasa wa Italy, Roberto Mancini akiwa na klabu ya Man
City, amesema anahofu sana juu ya uwezo wa kocha wake huyo wa zamani, hasa anapowaandaa
wachezaji wake na michezo mikubwa.
England kesho Jumapili itawavaa
Italy katika mchezo wa fainali wa michuano ya Euro 2020, itakayopigwa kwenye
uwanja wa Wembley nchini England.
Akizungumzia uwezo wa Mancini,
Richards amesema: “Mancini ni miongoni mwa makocha wenye uwezo mkubwa sana wa
kutengeneza saikolojia za wachezaji wake hasa kuelekea michezo mikubwa, hivyo
nadhani England wanapaswa kuwa makini sana kwenye mchezo huo wa fainali.
“Naweza kuyasema haya kwa kuwa nimewahi
kuwa chini yake, na nakumbuka vitu vingi kumhusu na mafanikio makubwa
niliyopata chini yake.”
0 COMMENTS:
Post a Comment