July 16, 2021

 


HUU ni msimu wanne mfululizo Simba 
wanakuwa mabingwa wa Tanzania Bara, si jambo dogo la kulipuuzia hata kidogo.

Simba wamekuwa mabingwa mara nne mfululizo wakiwa na kiwango bora zaidi ambacho huwezi kupinga hata kidogo.


Msimu mmoja kabla ya kuanza kuhesabu misimu yao minne, Simba walishika nafasi ya pili wakiwa wanawafuatia mabingwa Yanga ambao walipata pointi sawa kabisa lakini tofauti ya mabao ya kufunga, Simba wakiwa wanazidiwa mabao 10, Yanga akachukua zake ubingwa.


Baada ya hapo, Simba wakarejea na kubeba ubingwa mfululizo mara nne. Na kila msimu waliochukua ubingwa, wamekuwa bora katika kila idara.

Ukianza na kipa, Aishi Manula wa Simba amekuwa bora kwa muda wote wa misimu hiyo minne tokea alipojiunga na Simba akitokea Azam FC. Beki za pembani za Simba, mabeki wa kati wa Simba licha ya kwamba wamekuwa wakibadilika lakini wameifanya safu yao kuwa bora zaidi.



Ukienda katika kiungo, karibu kila msimu, kiungo cha Simba kilitengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga na kuzalisha pasi nyingi zaidi za mabao yaliyofungwa. 

Lakini safu ya ushambulizi ya Simba, ndiyo iliyofunga

mabao mengi zaidi kwa misimu yote minne.

Hata msimu huu, bila shaka mfungaji bora

atatokea Simba na John Bocco au Chris

Mugalu au Meddie Kagere ni kati ya

wanaonukia wakiwa wanashindana na

Prince Dube wa Azam FC ambaye

anasumbuliwa na majeraha.

Ukiachana na mafanikio haya katika Ligi Kuu

Bara, angalia katika misimu hii minne, Simba imeshiriki mara zote katika michuano ya kimataifa na imeweka rekodi ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili, imeweka rekodi ya kwenda robo fainali na imetengeneza jina lake Afrika kwa ukubwa sana na kuutangaza mpira wa Tanzania kwa kiwango cha juu sana.

Hapa ndipo ninataka kuwakumbusha viongozi wa klabu za soka au hata wadau wengine, kwamba haya waliyoyafanya Simba na kufikia hapa walipo, tusiyachukulie kama mambo fulani hivi mabaya au makosa au sehemu kama ya kitu kinachowaogopesha au kuwakera.

Watanzania wengi tuna tabia ya kukerwa na

mafanikio ya wenzetu, hatupendi kuona

wengine wanafanikiwa. Ukifurahia

mafanikio ya mwenzako, lazima utajiuliza

imekuwaje au amefanyaje na wewe utaanza kubadilika na kufanya jambo litakalochangia nawe kubadilika na kufanya vizuri.

Walipofikia Simba ni mfanikio na hatupaswi kuyachukulia kama aibu au adhabu kwetu.

Maana unaona wengi badala ya kukubaliana na Simba wanachokifanya, badala yake wanatengeneza sababu nyingi sana kutaka kuonyesha kinachofanyika si sawa au Simba wanabahatisha au wanapendelewa na kadhalika.

Tena viongozi ambao hawafikii mafanikio makubwa pamoja na kuwaahidi wanachama na mashabiki wao, ndio wanataka kuonyesha Simba hawana lolote na wanapendelewa.

Hili si jambo sahihi, badala yake viongozi hao wanapaswa kuguswa na mwendo waliokwenda nao Simba kwa misimu hiyo minne nao waweze kubadilika na kufanya jambo.

Tukubaliane, haliwezi kuwa jambo jepesi

kwamba licha ya kuwepo kwa timu nyingi

katika ligi hiyo, halafu wewe uwe

unachukua tu ubingwa kwa mara nne

mfululizo, lazima kutakuwa na mambo

muhimu kama ubinifu, uaminifu, ushirikiano

na umoja wa hali ya juu miongoni mwa

Wanasimba na hasa viongozi, wachezaji na

wanachama na mashabiki wao.

Hili ndilo nazishauri timu nyingine kuwa Simba hawalali wakaota na mafanikio hayo yakapatikana. Badala yake wanafanya kazi kwa kushirikiana na nia ya kutaka kufikia malengo yao. Walichonacho, tusikifanye kama kinatushambulia, badala yake kiwe sehemu ya kutuamsha, basi tubadilike, tujifunze na baadaye kufanya makubwa pia.

1 COMMENTS:

  1. Simba wameijenga timu yao kwa ajili ya kushindana Africa zaidi na si kwa ligi kuu peke yake na Kama timu ya Tanzania imeandaliwa kwa ya kushindania ubingwa wa Africa basi sioni kwa timu nyengine za Tanzania ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya kushindania ubingwa wa ligi kuu wakiipokonya simba ubingwa labda kwa figisu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic