KLABU ya Yanga imeonyesha heshima kwa kuamua kutoa mkono wa byebye kwa nyota wake, Haruna Hakizimana Niyonzima raia wa Rwanda.
Niyonzima ameagwa kwa heshima wakati Yanga ikiivaa Ihefu FC iliyokuwa inapambana kuhakikisha inashinda mechi yake dhidi ya Yanga ili ibaki Ligi Kuu Bara.
Yanga wameamua kumuaga Niyonzima kutokana na kazi kubwa aliyoifanya akiwa na kikosi cha Yanga ambacho kimemaliza msimu kikiwa katika nafasi ya pili lakini kimetinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.
Kiungo huyo amefanya mengi makubwa akiwa na kikosi cha Yanga, pamoja na kwamba alilazimika kuondoka mara moja na kurejea tena.
Mara moja, Niyonzima aliondoka na kujiunga na watani wa Yanga, Simba ambako baada ya hapo aliondoka na kwenda zake kwao Rwanda.
Wakati Yanga wakipika kikosi upya walimfuata tena Kigali ambako walizungumza naye na kufanikiwa kumrejesha. Amekuwa na mchango wake wakimaliza nafasi ya pili na fainali ya Kombe la Shirikisho.
Pamoja na yote, Niyonzima ameacha alama wakati wa ile Yanga ya Kampakampa tena ambayo ilikuwa ikitoa mateso kwa watani wake Simba kila mara.
Yanga ambayo ilikuwa ni burudani ya aina yake na kama unakumbuka, wakati anaingia pacha kwenye kiungo alikuwa ni Athuman Iddi Chuji na wakatikisa hasa. Wakati Chuji anaondoka Yanga, Niyonzima aliendelea kutamba na kwa wakati mwingine tena akasumbua akiwa na Thabani Kamusoko, wakiifanya Yanga kuwa gumzo hadi inatinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Bila shaka Yanga wanafanya jambo bora
kabisa la kumuaga raia huyo wa Rwanda
kutokana na kazi yake nzuri aliyoifanya
akiwa na Yanga kwa vipindi hivyo viwili
na anakuwa mmoja wa wachezaji wa
kigeni waliofanya vizuri zaidi katika Ligi
Kuu Bara.
Sasa anaondoka, heshima anastahili na
mimi ninauga mkono ingawa nina jambo
la kuuliza. Kwamba huu utaratibu mara
kadhaa, kuanzia kwa Yanga na baadhi ya
klabu zimekuwa zikiona sahihi kuwapa
heshima kwa kuwaaga au kuwapongeza
wachezaji wanapokuwa wanaondoka na
zaidi ni wale wa kigeni.
Kwa Yanga, inaweza kuwa imefanya kwa
wazalendo, lakini nawauliza tena,
hawaoni wachezaji kama Kelvin Yondani
pia walipaswa kuagwa kutokana na
mchango wao.
Mfano, wakati akiondoka Niyonzima,
ninaamini Yondani angekuwa tayari
ameishaagwa. Wakati fulani alikaa nje
bila ya timu na Yanga ilimaliza msimu
ambapo ingeweza kufanya jambo kwake
na kumuaga kwa kuwa alikuwa anastahili
kuagwa ili kuonyesha wanajali muda
wote wa mafanikio akiwa Yanga.
Wakati Niyonzima akitamba akiwa na
Chuji, Kamusoko na wengine. Yondani
ndiye alikuwa akishikilia jahazi la ulinzi la
kikosi cha Yanga. Tena alifanya kazi bora
akiwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
lakini hata baada ya kustaafu kwake,
Yondani aliendelea kupambana akiwa na
wachezaji kadha wa kadha mfano wa
Vicent Andrew ‘Dante’, Shaibu Ninja,
Said Makapu na wengine, akaendelea
kuwa tegemeo na mhimili wa ulinzi wa
klabu ya Yanga.
Hata wakati ule Niyonzima alipoondoka
kwenda kwao Rwanda, Yondani alikuwa
bado anaitumikia Yanga. Niyonzima
aliporejea na kujiunga na Simba, Yondani
bado alikuwa akipambana kukitumikia
kikosi cha Yanga. Leo kwenye kuagwa,
hakuwahi kupewa hiyo heshima.
Vizuri kufanya kama hicho kilichofanyika
kwa Niyonzima lakini vizuri zaidi
kuwakubuka waliofanya vizuri na kujituma kwa moyo wao wote kuhakikisha Yanga inapata inachotaka.
Tumeona hata Yanga mpya ambayo
ilibadili zaidi ya wachezaji 15, bado
haijafikia mafanikio ya waliyokuwa nayo
katika Yanga ya kina Yondani.
Kama ambavyo nimekuwa nikisema siku zote,
timu inapaswa kuendelea kujengwa na
msimu ujao unaweza kuwa bora zaidi
kwa Yanga kama watajipanga lakini
naendelea kuwakumbusha, Yondani ni
gwiji nchini, ni mmoja wa wachezaji bora
wazalendo kuwahi kutokea nchini na
anapaswa kupewa heshima yake.
Inawezekana isiwe kwa Yondani pekee
au Yanga pekee, nizikumbushe klabu nyingine, kuwaaga wachezaji wao kwa heshima na hasa wale waliojituma hasa kutaka klabu iwe bora na kushinda, wanapaswa kupewa heshima zao na
tusiwadharau kwa uzalendo wao na mara nyingi nimeona, wako viongozi wengi katika klabu zetu wana hisia za kuwadharau wachezaji wazalendo kwa
kuwa tu, wanaona kuwafanya waonekane wakubwa ni kama wao viongozi kujishusha.
Tena wakati mwingine, unakuta kiongozi
ana miaka miwili tu ndani ya klabu lakini
mchezaji ameitumikia klabu kwa zaidi ya
miaka sita hadi nane. Huu si uungwana
na haifai kuendelea, badilikeni.
Hebu tufafanulie zaidi katika hili,hivi ikitokea mfanyakazi wako akaamua kuondoka katika kampuni yako akaenda kampuni nyingine halafu akaamua kustaafu akiwa katika kampuni aliyohamia baada ya kutoka kwako je utafanya hafla ya kumuaga kwa kustaafu kwake?
ReplyDeleteKumbe niyonzima amestaafu?
DeleteAu kama huyo mfanyakazi aliondoka kwako akaenda sehemu nyingine na akawa anaendelea na kazi huko alipo je utalazimisha kumfanyia sherehe ya kustaafu? Au ulimaanisha send off?
ReplyDeleteKumbe niyonzima amestaafu?
DeleteKwani wewe ulielewa nini katika kumuaga Niyonzima?Inaonesha una kamasi kichwani badala ya ubongo.Neno kustaafu unalitafsiri vipi?
DeleteKamasi wanazo Utopolo maana mpaka leo wanaamini tar 23 watatangazwa mabingwa
DeleteYondani hakupewa heshima yeyote pale yanga. Na hii ni kama vile hawakuona mchango wake zaidi ya maslahi yao kutimizwa. Baada ya Yondani kushindwana na yanga kwasababu ya maslahi na akakaa msimu mzima bila timu Yanga walijenga mtima nyongo badala ya kumuaga kwa mema aliyofanya akiwa nao. Hii sio sawa ni udanzwi mtupu
ReplyDeleteNyie mliwahi kumuaga nani ambae aliondoka kwa zengwe
DeleteKwa kweli ni nani aliyeitumikia Yanga kwa kila mapenzi na uaminifu na kuipa mafanikio makubwa baina ya Niyonzima na Yondani?
ReplyDeleteYaani pamoja na kuihujumu timu yeye na kundi lake bado kuna nguchiro fulani wanataka tumpigie makofi
DeleteMlichoma jezi ya Niyonzima alivyoenda Simba na mkamuita msaliti...msijasahaulishe bhana
DeleteMbona mnateseka na timu sio yenu
DeleteKila kitabu na zama zake! Kila jambo lina mwanzo
ReplyDeleteMtoa posti acha uchochezi, ama vipi waulize Simba kwanini hawajamuaga Ibrahim Ajibu.
ReplyDeleteWe Saleh tumia akili hatahizo kidogo ulizonazo.kelvin aligoma kusaini yanga wanamuaga vipi? Au umezoea kuhongwa ili uchonganishe washabiki?acha uandishi wakijinga ishu ikowazi wenye akiliwote wameelewa Ila vilaza Kama wewe ni mtihani.,Hunajipya kaa kumya
ReplyDeleteYondani hajaondoka kwa maelewano mazuri, pia ukumbuke tim ilikua inapita ktk kipindi cha mpito.
ReplyDelete