July 7, 2021

 

BARAKA Majogoro kiungo wa Mtibwa Sugar amesema kuwa imani yao kubwa ni kuona kwamba timu hiyo inabaki ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22.

Nyota huyo ameongeza kwamba wachezaji wote pamoja na benchi la ufundi wamekuliana kuongeza juhudi zaidi ili kupata matokeo ambayo yatawafanya wabaki ndani ya ligi.

Mtibwa Sugar haijawa katika mwendo mzuri msimu huu na inahitaji kushinda mechi zake zote mbili ambazo imebakiwa nazo ili iweze kujinusuru kutoka janga la kushuka daraja.

Kwa sasa inanolewa  na Kocha Mkuu, Badru Mohamed ambaye alikuwa ndani ya Gwambina FC ila kwa sasa yupo viunga vya Mtibwa Sugar, Morogoro.

Nyota huyo amesema:"Tumekubaliana kufanya vizuri mechi ambazo zimebaki na imani yetu ni kuona kwamba tunabaki ndani ya ligi na hilo linawezekana mashabiki waendelee kutupa sapoti," .

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 11 na pointi zake  ni 38  baada ya kucheza mechi 32 imebakiwa na mechi mbili.

Pointi hizo haziwapi nafasi ya kubaki kwenye ligi ikiwa wataweza kupoteza mechi mbili za mkononi kwa sababu zinaweza kufikiwa na Coastal Union ya Tanga iliyo nafasi ya 17 na pointi 34.

Coastal Union imebakiwa na kete tatu mkononi ambapo ikishinda zote inaweza kufikia pointi za Mtibwa Sugar ambapo inaweza kufikisha jumla ya pointi 43 hivyo ni suala la kusubiri dk 90 zitaamua.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic