July 5, 2021






 MZEE wa Yanga ambaye yupo kwenye baraza la Wazee, Mzee Mpili amesema kuwa kwa sasa wapo juu baada ya kuchukua pointi tatu na kituo kinachofuata ni Kigoma.

Yanga inatarajiwa kukutana na Simba kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho inayotarajiwa kuchezwa Julai 25, Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma.

Mpili ambaye alikuwa anatamba tangu awali kwamba Yanga itawafunga Simba ameweka wazi kwamba mpira Yanga upo na kituo kinachofuata ni Kigoma huko hawezi kuwaambia kwa sasa nini kitatokea.

"Matokeo tumeyapata na kama tumeomba matokeo tumepata basi tupo juu leo tumechukua pointi tatu tupo juu na pointi 70 na awali hesabu zetu ilikuwa kuchukua ubingwa.

"Watu wanaona mpira hatuna, sisi ilipaswa tuchukue ubingwa mwaka huu na unaona kwamba kwa sasa tupo juu. Watu ambao nipo nao ni sababu inayofanya tuwe tunajiamini hivyo tusubiri na tuone," amesema.

Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 70 baada ya kucheza mechi 32 Simba ipo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 73 baada ya kucheza mechi 30.

5 COMMENTS:

  1. Huyu kigagula sasa tambo juu. Tuone kama ataendelea kutamba na uchawi wake mechi zote

    ReplyDelete
  2. Uchawi ndo maana wanaishia kuwa wa mchangani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wale paka weusi na kuku mnaochinja uwanjani ni nini? Huwa ni maombi au?

      Delete
    2. Wenzenu wanaloga kimataifa ninyi mnaloga kitaifa, kweli akili matope

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic