July 27, 2021


 KIUNGO Mshambuliaji wa Simba raia wa Ghana, Bernard Morrison, amekabidhiwa kitita cha shilingi Ml 1, kutoka kampuni ya Emirate Alluminium baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Mwezi Juni.

Nyota huyo mzee wa kuchetua ametwaa tuzo hiyo baada ya kura za mashabiki kupigwa kwa wingi kupitia mitandao ya kijamii.

Alitwaa tuzo huyo baada ya kuwashinda wachezaji wenzake ambao ni Luis Miquissone na nahodha wake John Bocco, ambapo walikuwa wakiwania tuzo hiyo pamoja.

 

Tuzo hiyo imekuwa ikitolewa na Kampuni ya Emirate Alluminum kila mwezi, huku mchakato wa kumpata mshindi huendeshwa na Simba kupitia kura za mashabiki wa klabu hiyo.

3 COMMENTS:

  1. Hizi tuzo jamani bora zingesubiri kesi iishe maana na zenyewe mnaweza kuambiwa mzirudishe kudadadeki!

    ReplyDelete
  2. Haya ndio yanayowarusha akili matopolo kila wanaposikia kutukuka kwa Morrison hujisahau na kuisahau timu yao na kumwacha Mnyama azoe makombe. Mzee Mpili lazima uyashugulikie haya kwa maslahi ya timu yako au daima mtajikuta mikono mtupu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic