KIUNGO mshambuliaji mpya wa klabu
ya Azam, Charles Zulu amefunguka kuwa miongoni mwa sababu kubwa za yeye kusaini
ndani ya kikosi cha Azam, ni kuvutiwa na viwango vya Clatous Chama, Rally
Bwalya na Obrey Chirwa ambao ni raia wa Zambia wanaofanya vizuri hapa nchini.
Zulu alikamilisha usajili wake
ndani ya kikosi cha Azam juzi Jumapili akitokea ndani ya klabu ya Cape Town
City ya nchini Afrika Kusini, baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Nyota huyo wa zamani wa wababe wa
soka wa Zambia, klabu ya Zanaco amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Azam
ambapo ataanza rasmi kutumika mwanzoni mwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara wa
2021/22.
Akizungumza baada ya kusaini Azam, Zulu amesema: “Nimefurahi kutua ndani ya kikosi cha
Azam, kwangu hii ni hatua kubwa katika maisha yangu ya soka, na naamini
nimekuja kuongeza thamani ndani ya timu hii. malengo yangu makubwa ni kushinda
makombe.
“Nimevutiwa kujiunga Azam kwa sababu ya nafasi
ya kushiriki michuano ya Afrika msimu ujao, lakini pia kutokana na mahusiano
mazuri niliyonayo na baadhi ya wachezaji wa Zambia ambao wanafanya vizuri hapa
Tanzania kama vile Clatous Chama, Rally Bwalya na Obrey Chirwa.”
0 COMMENTS:
Post a Comment