July 28, 2021


BAADA ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Wanamsimbazi, Kipa wa Yanga SC Raia wa Kenya Farouk Shikalo, amesema kuwa wao kama timu mipango yao ni katika msimu ujao kwani wamejipanga kuja kivingine mara baada ya msimu huo kuanza.

Shikalo mwenye uraia wa Kenya kwa sasa ndiye kipa namba moja wa Yanga  ambapo amepata nafasi ya kucheza katika michezo ya mwisho baada ya Metacha kusimamishwa kuitumikia klabu hiyo, huku Ramadhani Kabwili akiwa chaguo la pili ndani ya Yanga.

Akizungumzia mipango yao, Shikalo amesema kuwa kitu wanachokipa nafasi kubwa kwa sasa ni mipango ya kuelekea msimu ujao kwa ajili ya mchezo wa ngao ya Jamii na mashindano ya kimataifa.

“Malengo yetu kwa sasa ni kuhakikisaha tunafanya vizuri msimu ujao kwa kuwa msimu huu umeisha na hatujafikia malengo yetu.

“Tunajipanga katika mashindano ya kimataifa  yaliyopo mbele yetu hivi karibuni pia, tutahakikisha tunarekebisha makosa ya msimu huu na kuchukua ubingwa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii pamoja na mashindano ya  Cecafa,” amesema Shikalo.

 

7 COMMENTS:

  1. Siku yanga wakiingia kucheza na simba na sio kungfuu ndio watajua kwa nini uwezo wao uko chini. Wao wanachojua ni kukamia tuu na kutanguliza vitisho kwa marefa ili wawatoe umakini wafanikishe gwaride lao. Waende hivyo kimataifa watazioga redcard.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama kungfu za Boko, Mugalu na yule mganda bwana maguvu au?

      Delete
  2. Huyu nae chiz,kila msimu hayo hayo maneno,,eti tunakuja kivingne,tumechoka hayo maneno

    ReplyDelete
  3. Jiulizeni kwani Yanga wameshachukua ubingwa mara ngapi? Ukanjanja tupu!

    ReplyDelete
  4. Huko miala ya nyuma kulikuwa hakuna umakini

    ReplyDelete
  5. Yupo sahihi huwez sema msimu ujao tunafanya vby

    ReplyDelete
  6. Kweli Wapenzi wa mikia wengi kwa asili siyo Watoto wa baba zao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic