July 27, 2021


 KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania amesema kuwa anashangazwa na uwezo wa wachezaji wake alionao kwa sasa kwa namna ambavyo wanafanya vizuri ndani ya uwanja.

Leo Julai 27, Uwanja wa Bahir Dar, katika mashindano ya CECAFA 2021 yanayofanyika nchini Ethiopia, timu ya taifa ya Tanzania, chini ya miaka 23 imefanikiwa kutinga hatua ya fainali.

Ni ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sudan Kusini ambalo limepachikwa na Kelvin Nashon kwa pigo huru la faulo akiwa nje ya 18 ilikuwa dakika ya 64 na kuifanya timu hiyo kuibuka na ushindi.

Kima amesema:"Ninashangazwa na uwezo wa wachezaji wangu hasa ndani ya uwanja, lakini kwangu ninaona ni jambo jema kwani tunahitaji ushindi na ushindani ni mkubwa," .

Fainali inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ambapo itakuwa ni kati ya Tanzania dhidi ya  Burundi.

Timu hiyo ilipocheza na Uganda ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na ilishinda bao 1-0 ilipocheza na DR Congo.

5 COMMENTS:

  1. Hongereni sana vijana wetu kwa kupeperusha vyema bendera ya Nchi yetu. Kazeni buti mrudi na kombe

    ReplyDelete
  2. Mwandishi muombe radhi Kocha kwa kumwita Kima

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wa lasaba wanatisha "no editing before posting" ni kanyaga twende

      Delete
  3. Haya mashindano ya wagonjwa hayana maana tukipeleka hivyo timu AFCON U23 utashangaa wanapigwa zote

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic