BAADA ya subira ya muda mrefu na mizengwe ya hapa na pale
kuhusiana na mchezo wa mzunguko wa pili wa dabi ya Kariakoo, hatimaye yamebaki
masaa machache kuzielekea dakika 90 zitakazoamua ubishi huo.
Mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam
kwa mara ya kwanza ulipangwa kuchezwa Februari 20, mwaka huu kabla ya
kuahirishwa mpaka Mei 8, ambapo mabadiliko ya ghafla ya ratiba yakaufanya
mchezo huu kupelekwa mbele mpaka kesho Julai 3.
Mara zote kuelekea mchezo huu, tambo huwa nyingi vijiweni
ambapo mashabiki wa kila upande wamekuwa wakitambiana kuibuka na pointi tatu
muhimu kwenye mchezo huo, huku wengine wakienda mbali na kubashiri idadi ya
mabao ambayo wanahisi timu zao zitashinda.
Kwa mashabiki hili halishangazi sana kwa kuwa ni haki yao ya
msingi kabisa kama tu haivuki mipaka, na kukiuka sheria na kanuni za soka na
zile za nchi kiujumla.
Hivyo licha ya uhalali wa tambo hizo za mashabiki kitu cha
msingi kwao ni kuwa watulivu, na kuwaacha walimu wafanye majukumu yao, huku
jukumu lao kama mashabiki likiwa ni kusapoti timu na si kingine.
Kwa wachezaji, huu ni wakati wao wa kupigania heshima za
mashabiki wao kwani ugonjwa wa mashabiki ni kuona mpira mzuri, kama ni pira
gwaride au pira sambusa vyovyote vile.
Masuala ya kugeuza viwanja vya soka kuwa ulingo ni kitu
ambacho hatukitarajii kutoka kwa mashabiki kwani ulingo anapaswa kuachiwa kwa
mabondia kama, Twaha Kiduku na Dulla Mbabe huku liwe suala la burudani tu.
Taifa la Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayosifika kwa
kudumisha amani na upendo hivyo ninaamini kwamba hakutakuwa na ugomvi kuanzia
kwa mashabiki na wachezaji pia.
Chondechonde mashabiki hampaswi kuja na matokeo yenu kwenye
mchezo huu, kwa kuwa mara zote mchezo wa dabi huwa na kawaida ya matokeo ya
kushangaza na kustaajabisha.
Ligi ya msimu huu imekuwa na ushindani wa aina yake, kiasi
cha kuwepo na ugumu kutabiri matokeo ya dakika 90.
Waamuzi pia tunaomba msimamie misingi ya haki katika
kusimamia sheria 17 za soka, kwani kumekuwa na tabia ya makosa ya
kujirudiarudia.
Miongoni mwa mitihani migumu kwa waamuzi ni huu wa kuchezesha
dabi, ambayo inafuatiliwa na wapenzi mbalimbali wa soka. Umakini unahitajika
katika kufuata sheria zote 17 za mchezo wa soka.
Ikitokea mwamuzi akaboronga ni rahisi kuzomewa ama
kusababisha vurugu, jambo ambalo hakuna Mtanzania anayependa kuona tunafikia
hatua hiyo.
Masuala ya kuboronga makusudi kwa kuwa kuna adhabu eti za
kufungiwa ama kuonywa.
Wapo wachezaji ambao wamepania kufanya maajabu, lakini
wanapaswa kuacha kuingia na matokeo yao, na kuamini kwamba matokeo yatapatikana
ndani ya dakika 90.
Kikubwa ni maandalizi kwa timu zote kuanzia benchi la ufundi.
Naamini kama waamuzi wa mchezo huu watatenda haki basi kuna uwezekano mkubwa
kila kitu kikaenda sawa lakini makosa yao yanaweza kupelekea maafa.







This man always Ana I favour KARIA fc pls usituzuge
ReplyDeleteTeam Karia vipi..... Mmeona mtuwekee picha ya kijani ili iweje..... Mikia bhana yaani nyie si mna kikosi Bora....mbona mnaahidi wachezaji pesa nyingi mkitufunga wakati team yetu ni mbovu
ReplyDeleteKaria FC?? Duh, mbona watu wanapenda sana kujisahaulisha? Kama ni hivyo, nawakumbusha kulikuwa pia na zama za 'Malinzi FC', au mlikuwa wengine hamjazaliwa nini?
ReplyDeleteteam karia iliwapa yanga penati isiyostahili mechi ya kwanza
ReplyDelete