July 2, 2021

 

BAADA ya subira ya muda mrefu na mizengwe ya hapa na pale kuhusiana na mchezo wa mzunguko wa pili wa dabi ya Kariakoo, hatimaye yamebaki masaa machache kuzielekea dakika 90 zitakazoamua ubishi huo.

 

Mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kwa mara ya kwanza ulipangwa kuchezwa Februari 20, mwaka huu kabla ya kuahirishwa mpaka Mei 8, ambapo mabadiliko ya ghafla ya ratiba yakaufanya mchezo huu kupelekwa mbele mpaka kesho Julai 3.

 

Mara zote kuelekea mchezo huu, tambo huwa nyingi vijiweni ambapo mashabiki wa kila upande wamekuwa wakitambiana kuibuka na pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo, huku wengine wakienda mbali na kubashiri idadi ya mabao ambayo wanahisi timu zao zitashinda.

 

Kwa mashabiki hili halishangazi sana kwa kuwa ni haki yao ya msingi kabisa kama tu haivuki mipaka, na kukiuka sheria na kanuni za soka na zile za nchi kiujumla.

 

Hivyo licha ya uhalali wa tambo hizo za mashabiki kitu cha msingi kwao ni kuwa watulivu, na kuwaacha walimu wafanye majukumu yao, huku jukumu lao kama mashabiki likiwa ni kusapoti timu na si kingine.

 

Kwa wachezaji, huu ni wakati wao wa kupigania heshima za mashabiki wao kwani ugonjwa wa mashabiki ni kuona mpira mzuri, kama ni pira gwaride au pira sambusa vyovyote vile.

 

Masuala ya kugeuza viwanja vya soka kuwa ulingo ni kitu ambacho hatukitarajii kutoka kwa mashabiki kwani ulingo anapaswa kuachiwa kwa mabondia kama, Twaha Kiduku na Dulla Mbabe huku liwe suala la burudani tu.

 

Taifa la Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayosifika kwa kudumisha amani na upendo hivyo ninaamini kwamba hakutakuwa na ugomvi kuanzia kwa mashabiki na wachezaji pia.

 

Chondechonde mashabiki hampaswi kuja na matokeo yenu kwenye mchezo huu, kwa kuwa mara zote mchezo wa dabi huwa na kawaida ya matokeo ya kushangaza na kustaajabisha.

 

Ligi ya msimu huu imekuwa na ushindani wa aina yake, kiasi cha kuwepo na ugumu kutabiri matokeo ya dakika 90.

 

Waamuzi pia tunaomba msimamie misingi ya haki katika kusimamia sheria 17 za soka, kwani kumekuwa na tabia ya makosa ya kujirudiarudia.

 

Miongoni mwa mitihani migumu kwa waamuzi ni huu wa kuchezesha dabi, ambayo inafuatiliwa na wapenzi mbalimbali wa soka. Umakini unahitajika katika kufuata sheria zote 17 za mchezo wa soka.

 

Ikitokea mwamuzi akaboronga ni rahisi kuzomewa ama kusababisha vurugu, jambo ambalo hakuna Mtanzania anayependa kuona tunafikia hatua hiyo.

 

Masuala ya kuboronga makusudi kwa kuwa kuna adhabu eti za kufungiwa ama kuonywa.

 

Wapo wachezaji ambao wamepania kufanya maajabu, lakini wanapaswa kuacha kuingia na matokeo yao, na kuamini kwamba matokeo yatapatikana ndani ya dakika 90.

 

Kikubwa ni maandalizi kwa timu zote kuanzia benchi la ufundi. Naamini kama waamuzi wa mchezo huu watatenda haki basi kuna uwezekano mkubwa kila kitu kikaenda sawa lakini makosa yao yanaweza kupelekea maafa.

 

4 COMMENTS:

  1. This man always Ana I favour KARIA fc pls usituzuge

    ReplyDelete
  2. Team Karia vipi..... Mmeona mtuwekee picha ya kijani ili iweje..... Mikia bhana yaani nyie si mna kikosi Bora....mbona mnaahidi wachezaji pesa nyingi mkitufunga wakati team yetu ni mbovu

    ReplyDelete
  3. Karia FC?? Duh, mbona watu wanapenda sana kujisahaulisha? Kama ni hivyo, nawakumbusha kulikuwa pia na zama za 'Malinzi FC', au mlikuwa wengine hamjazaliwa nini?

    ReplyDelete
  4. team karia iliwapa yanga penati isiyostahili mechi ya kwanza

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic