July 7, 2021

 


MFADHILI wa Klabu ya Yanga, Ghalib Salim Mohamed ‘GSM’ ameripotiwa kutoa Shilingi milioni 500 kwa wachezaji wa klabu hiyo, baada ya kuitungua Simba, Jumamosi Julai 3 Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam bao 1-0.

 

GSM imeripotiwa kutoa zawadi hiyo, kama kutimiza ahadi yake kwa wachezaji wa Yanga ambao alikutana nao kabla ya kukutana na Simba na kuwaahidi endapo watashinda atawapatia kiasi hicho cha pesa.

 

Taarifa kutoka kwa wachezaji wa timu hiyo ni kwamba hawakutaka kupishana na fedha hizo na kwamba walitambua viongozi wao wanataka ushindi nao wakafanya kweli.

 

Hesabu za harakaharaka ni kwamba kuna uhakika kila mchezaji haitapungua kiasi cha Shilingi milioni 20 katika ahadi hiyo ya vigogo wa klabu yao.

 

Ahadi hiyo inaweza kuwashtua wengi kutokana na kuwa ndio ahadi kubwa kwani hakuna klabu imewahi kutoa ahadi kubwa katika mchezo wa Ligi Kuu Bara zaidi ya hiyo kwa msimu huu 2020/21.

 

Bao la ushindi la Yanga katika mchezo wa Jumamosi lilifungwa na kiungo mzawa Zawadi Mauya dakika ya 11, kwa kupiga shuti kali lililombabatiza beki wa pembeni wa Simba SC, Shomari Kapombe.

 

Ushindi huo umeiwezesha Yanga kufikisha alama 70, huku ikisalia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Simba ikiwa kileleni kwa kumiliki alama 73.

3 COMMENTS:

  1. Vzr km ahadi imetimizwa, kujituma inakuwa rahisi

    ReplyDelete
  2. Safi sn ila tangu mwanzo mngelipa wachezaji madai yao kwa wakati ingefaa zaidi huenda hata ubingwa tungepata

    ReplyDelete
  3. IMEVUJA: Julai 25 mtu anapigwa 4G

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic