TAARIFA za ndani kutoka ndani ya klabu ya Simba zinaeleza kuwa klabu ya soka ya As Far Rabat ya nchini Morocco, imeingia kwenye vita na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika jitihada za kuhitaji saini ya kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama.
Awali ni viongozi wa klabu ya Kaizer Chiefs ndiyo walikuwa wa kwanza kuonyesha uhitaji wa kuisaka saini wa Clatous Chama, ambaye amekuwa gumzo msimu huu kutokana na kuonyesha uwezo mzuri katika michuano ya Ligi Kuu Bara na ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Chama msimu huu kwenye Ligi Kuu pekee amehusika kwenye mabao 23, akiwa amefunga mabao nane na kuasisti mara 15.
Vyombo vya habari nchini Morocco vimeripoti kuwa Chama atasaini AS FAR Rabat, kutokana na jina lake kupendekezwa na aliyekuwa kocha wake ndani ya Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck.
Akizungumzia kuhusu taarifa hizo, Mkuu wa maudhui wa klabu ya Simba, Ally Shatry amesema: “Kumekuwa na taarifa nyingi kuwahusu baadhi ya wachezaji wetu nyota, ambao wameonekana kufanya vizuri msimu huu, Simba haina pingamizi lolote la kumzuia mchezaji ikiwa taratibu stahiki zitafuatwa.
“Lakini pia hayo yatafanikiwa ikiwa tu viongozi hasa wa benchi la ufundi watakubaliana na ofa hiyo, kwa kuwa malengo yetu ni kusalia na wachezaji wetu wote bora kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22.
“Kwa kuwa kwa sasa tupo likizo,
nisingependa kuzungumzia hilo sana mpaka pale tutakaporejea.”
Leteni Pesa sisi uto wazee wakubana
ReplyDelete